Klabu ya Tabora United imefungiwa kusajili mpaka itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wa klabu hiyo, Jean Didie Touya.
Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu baada ya mchezaji Jean Didie Touya kufanikiwa kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo.
Mchezaji huyo raia wa Cameroon alifingua kesi FIFA akidai malipo ya malimbikizi ya mishahara na fidia ya kuvunjiwa mkataba
Klabu hiyo ilitakiwa iwe imewalipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa lakini hawakutekeleza hukumu hiyo.
Wakati FIFA imefungia klabu hiyo kufanya uhamisho kwa wachezaji wa kimataifa Shirikisho la Soka la Tanzania "TFF" limezuia klabu hiyo kufanya uhamisho wa ndani.
Pia TFF imezikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo imeingia na wachezaji na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili.

Post a Comment