ISHOWSPEED YAMKUTA MAZITO FAINALI YA SUPER CUP ALGERIA



Streamer maarufu duniani, IShowSpeed, amelazimika kuondolewa uwanjani kwa ulinzi mkali wakati wa fainali ya Super Cup ya Algeria, Januari 17, 2026. 

IShowSpeed alikuwa miongoni mwa wageni waliokuwepo kushuhudia mchezo huo mkubwa uliopigwa katika Uwanja wa Nelson Mandela, lakini hali ilibadilika ghafla baada ya baadhi ya mashabiki kuanza kumlenga kwa kurusha vitu mbalimbali.

Kutokana na mazingira yasiyo salama, walinzi wa usalama walichukua hatua ya haraka kumtoa uwanjani kwa ajili ya kumlinda. 

Akiwa anaondolewa, IShowSpeed alisikika akiuliza kwa mshangao:
“Nimefanya nini vibaya? Nimekuja tu kuangalia mechi.”

Katika uwanja, mchezo huo wa fainali ya Super Cup ya Algeria ulimalizika kwa MC Alger kuibuka na ushindi wa bao 1-0, matokeo yaliyowawezesha kubeba taji hilo muhimu la msimu.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post