Shirikisho la soka Barani Afrika limetangaza rasmi kufuta Michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN).
Uamuzi huo ulithibitishwa na Rais wa CAF, Dkt. Patrice Motsepe wakati wa mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika Morocco Jumamosi, Januari 17.
Dkt. Motsepe alieleza moja kwa moja sababu ya hatua hiyo, akielezea shindano hilo kuwa haliwezi kutegemewa kifedha.
Rais wa CAF pia alifichua kuwa kalenda ya soka ya bara hilo itafanyiwa mabadiliko makubwa, huku mashindano mapya yakipangwa kuchukua nafasi ya CHAN.
Dkt. Motsepe pia aligusia uhusiano mpana wa CAF na mashirika ya soka duniani, akisisitiza haja ya uhuru na ushirikiano badala ya migawanyiko.


Post a Comment