Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeanza vyema michuano ya CHAN 2024 baada ya kuichapa Burkina Faso mabao 2-0 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa na kujinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 60.
Kiasi hicho kimetolewa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ametoa Milioni 20 zilizokabidhiwa na Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa. Viongozi wengine ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi (Milioni 20) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila (Milioni 20).
Baada ya kukabidhi fedha hizo, viongozi hao wameipongeza Stars kwa kuleta furaha kwa Watanzania na kuonyesha mwanzo bora wa mashindano.
Kocha wa Stars, Hemed Suleiman Ali ‘Morocco’ amemshukuru Rais Samia kwa hamasa yake kwa timu hiyo na kuahidi kuendeleza ushindi kwenye michezo ijayo.
Stars sasa inajiandaa kuvaana na Mauritania katika mchezo wa pili utakaopigwa Jumatano, Agosti 6, 2025.


Post a Comment