Mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba, Crescentius Magori amesema kuwa hawajasusa mechi ya #KariakooDerby bali hadi ligi, Simba haitoshiriki mpaka waliohusika na tukio la wao kushindwa kuingia uwanja na kufanya mazoezi ya mwisho waadhibiwe.
"Siyo mechi ya kesho tu (leo) hatuchezi Ligi mpaka hawa wapuuzi walishiriki kwenye huu upuuzi waadhibiwe"
Simba SC imetangaza kutoshiriki mchezo wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Yanga SC kutokana na kile ilichodai ukiukwaji wa taratibu na vurugu zilizotokea kabla ya mechi.
"Timu ngeni ina haki ya kufanya mazoezi kwenye uwanja wa mechi angalau mara moja kabla ya siku ya mchezo. Hata hivyo, Simba ilinyimwa haki hiyo licha ya kufika kwa wakati."
Katika hali hiyo ya sintofahamu, taarifa imesema Meneja wa Uwanja alidai hana maelekezo ya kuruhusu mazoezi bila kibali cha kamishna wa mchezo. Pamoja na kamishna kufika, mabaunsa wa Yanga walivamia msafara wa Simba na kuzua vurugu, hali iliyozuia timu hiyo kuingia uwanjani kwa mazoezi.
Taarifa imesema jitihada za Simba SC kupata suluhisho zilidumu kwa zaidi ya saa mbili bila mafanikio, na hatimaye klabu ililazimika kuondoka kwa sababu za kiusalama.

Post a Comment