FANYENI YOTE AFRIKA NZIMA INASUBIRI DERBY YA KARIAKOO




Baada ya klabu ya Simba kutangaza, kutoshiriki mchezo wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Yanga SC kutokana na kile ilichodai ukiukwaji wa taratibu na vurugu zilizotokea kabla ya mechi.

Mkurugenzi wa Sheria wa Klabu ya Yanga, Simon Patrick ameibuka na kutoa neno juu ya sakata ilo "Kwa mujibu wa kanuni, ni kweli kwamba timu ngeni ina haki ya kufanya mazoezi angalau mara moja kabla ya mechi.

Hata hivyo, kwa kuwa ligi yetu inaendeshwa kwa busara, na ikizingatiwa kuwa katika mzunguko wa kwanza Klabu ya Yanga ilinyimwa haki ya kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi, basi hakuna uhalali wa kuruhusu wenzetu kufanya mazoezi ili kuepuka upendeleo wa aina yoyote (“double standard”). Kama mamlaka zingekuwa makini katika kusimamia kanuni kwa kiwango sawa na wanavyofanya katika kutoa faini kwa vilabu na kuwafungia wasemaji, hali hii isingekuwepo. 

NB: Fanyeni yote Afrika nzima inasubiria derby ya Kariakoo.


 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post