Winga wa Manchester United, Amad Diallo anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa miezi mitatu na pengine mpaka mwisho wa msimu baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu (ankle) akiwa kwenye mazoezi ya klabu hiyo inayojiandaa kuivaa Tottenham Hotspur.
Amad (22) raia wa Ivory Coast amethibitisha kupata jeraha hilo huku akionesha kusikitishwa na hali hiyo ambapo amesema atakuwa nje ya uwanja kwa muda na ataipa sapoti timu hiyo akiwa nje ya uwanja.
“Kwa bahati mbaya, nitakuwa nje kwa muda kutokana na jeraha. Nitarudi nikiwa na nguvu kuliko wakati wowote! Ni muda wa kuwaunga mkono vijana nikiwa nje ya uwanja.” — ameandika Amad kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii.
Man United pia itawakosa viungo Kobbie Mainoo, Manuel Ugarte na Toby Collyer kwenye mchezo dhidi ya Spurs ambao wataungana na Lisandro Martinez, Luke Shaw, Mason Mount na Jonny Evans kwenye meza ya matibabu.

Post a Comment