Baada ya producer S2kizzy kusema kuwa yeye ndiye producer bora kwa kizazi chake na asifananishwe na producer mwingine yeyote hapa Afrika Mashariki na kwamba yeye ni producer namba mbili wa muda wote.
Hii iliibua mjadala mkubwa mitandaoni ambapo Msanii wa Hip Hop nchini, Songa amesema S2kizzy hana ukubwa huo na sio mkali kihivyo bali anabebwa tu na ukali wa wasanii anaofanya kazi ila beats zake za kawaida sana
"Hits anazosema S2kizzy mpaka kujiita G.O.A.T ni kwa sababu ya wasanii aliofanya nao kazi, ukitoa sauti za wasanii hao zibaki beats tupu halafu ulinganishe na beats za producers wengine hapo ndipo kasheshe itapokuwepo" ameandika Songa kupitia mtandao wa X.

Post a Comment